TATIZO LA UKE KUWA MKAVU, CHANZO NA MATIBABU
CHANZO CHA TATIZO
Tatizo la uke kuwa mkavu linawakumba sana watu waliofikia ukomo wa hedhi (Menopause) Kutokana na sababu kwamba mwanamke anapofikia kipindi hiki mwili unapunguza au kuacha kutengeneza hormone hii ya estrogen.
👉Kuzaa na kunyonyesha. Kipindi hiki mwili unazalisha hormone ya maziwa (prolactin hormone) ambayo pia inazuia kuzalishwa kwa hormone ya estrogen.
👉Matibabu ya saratani. (Tiba ya mionzi na dawa za saratani)
👉Kutolewa mifuko ya mayai( ovaries)
UCHUNGUZI
Unapopata muwasho,au maumivu wakati wa tendo la ndoa na kuona uke wako ni mkavu vyema ukafika hospitali au ukawasiliana na daktari.Daktari atakuuliza maswali muhimu ili kubaini chanzo cha tatizo na atakufanyia vipimo na uchunguzi na atajua dawa gani inafaa.
MATIBABU
Matibabu yaliyozoeleka katika hili tatizo la ukavu ukeni ni kwa kutumia Estrogeni za kupaka au kupachika ukeni (topical estrogen),
Pia estrogen inaweza kuwa kaitka miundo mbali mbali kama ifatavyo:
Ring (estring) Hii inakua ni kitu cha duara kama pete ambacho mtu anawekewa ukeni,kinakua kinazalisha hormone ya estrogen,na kinabadilishwa kila baada ya miezi mitatu
Dawa za kupaka /cream (Estrace na Prematin)
Dawa hizi unapaka ukeni kila siku kwa muda wa wiki mbili.
Vidonge (Vagifem),Vidonge hivi ni bya kupachika ukeni vinakua na kifaa chake maalumu cha kusaidia kuviingiza ukeni.Unapachika kidonge kimoja kwa siku ndani ya muda wa week mbili.
MUHIMU:
Dawa zenye Estrogen zinakuwa na maudhi madogo madogo (side effects) kama matiti kuvimba na kuuma na dawa za estrogen hazipaswi kutumiwa na watu wenye matatizo yafuatayo:
Saratani ya matiti
saratani ya shingo ya kizazi
Wajawazito na wanonyonyesha.
You can follow @biturojr.
Comments
Post a Comment