KUMBEMENDA MTOTO NI NINI?
Kumbemenda mtoto ni mtoto kutokua vizuri ikidhaniwa kutokea kutokana na mama anayenyonyesha mtoto kukutana kimapenzi na mwenzi wake hasa kipindi mtoto bado ni mchanga na ananyonyeshwa.
Hii ni dhana iliyopo katika jamii mbalimbali, na inadhaniwa hutokea kwa sababu mtoto kunyonya maziwa yenye mbegu za kiume zilizoingia kwenye maziwa baada ya kufanya mapenzi.
JE, KUNA UKWELI WOWOTE?
HAPANA. kiukweli na kiutaalamu dhana hii si sahihi kabisa!
kufanya mapenzi na mwenzi wako baada ya kujifungua hakuwezi kusababisha afya ya mtoto kuzorota. mwanamke anapokutana na mwanaume kimapenzi, shahawa huingia kwenye tumbo la uzazi na kubaki huko. haziingii kwenye damu wala haziwezi kufika kwenye maziwa.
NI BAADA YA MUDA GANI MWANAMKE ALIYEJIFUNGUA ANAWEZA KUFANYA MAPENZI?
unaweza kuanza kufanya mapenzi tena baada ya maji maji yenye damu ya uke (lochia) kuacha kutoka ambayo ni kama wiki 3 mpaka 4 baada ya kujifungua, na wewe kujisikia vizuri na kuwa tayari kushiriki mapenzi.
pia, mnaweza kusubiri mpaka wiki 6 zipite toka ulivyojifungua.
JE, KUNA ATHARI YOYOTE YA KUFANYA MAPENZI BAADA YA KUJIFUNGUA?
Kufanya mapenzi baada ya kujifungua hakuwezi kuleta madhara kwa mtoto endapo hamna maambukizi ya magonjwa kama virusi vya ukimwi (vvu).
ikiwa mwanaume ana vvu anaweza kumuambukiza mama na kisha mtoto kuambukizwa kupitia maziwa ya mama.
Ikiwa mnafanya mapenzi kabla ya damu damu ya ukeni kukata, maambukizi ya bakteria yanaweza kutokea kwenye tumbo la uzazi (endometritis).
Pia kuna uwezekano wa mama kupata ujauzito miezi 6 ya kwanza ya kunyonyesha.
NINI KINASABABISHA AFYA YA MTOTO KUZOROTA?
Kukosa maziwa ya mama ya kutosha
Mtoto kushindwa kunyonya vizuri
Matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo (congenital heart diseases).
Kuanzishiwa vyakula vya ziada mapema, kabla mtoto hajafikisha miezi 6 au vyakula visivyo na viritubisho vya kutosha.
Homa, nimonia na maambukizi ya mfumo wa mkojo (uti) za mara kwa mara.
Maambukizi ya magonjwa kama virusi vya ukimwi (vvu) au kifua kikuu.
You can follow @biturojr
Comments
Post a Comment