TATIZO LA UKE KUWA MKAVU, CHANZO NA MATIBABU
CHANZO CHA TATIZO Tatizo la uke kuwa mkavu linawakumba sana watu waliofikia ukomo wa hedhi (Menopause) Kutokana na sababu kwamba mwanamke anapofikia kipindi hiki mwili unapunguza au kuacha kutengeneza hormone hii ya estrogen. πKuzaa na kunyonyesha. Kipindi hiki mwili unazalisha hormone ya maziwa (prolactin hormone) ambayo pia inazuia kuzalishwa kwa hormone ya estrogen. πMatibabu ya saratani. (Tiba ya mionzi na dawa za saratani) πKutolewa mifuko ya mayai( ovaries) UCHUNGUZI Unapopata muwasho,au maumivu wakati wa tendo la ndoa na kuona uke wako ni mkavu vyema ukafika hospitali au ukawasiliana na daktari.Daktari atakuuliza maswali muhimu ili kubaini chanzo cha tatizo na atakufanyia vipimo na uchunguzi na atajua dawa gani inafaa. MATIBABU Matibabu yaliyozoeleka katika hili tatizo la ukavu ukeni ni kwa kutumia Estrogeni za kupaka au kupachika ukeni (topical estrogen), Pia estrogen inaweza kuwa kaitka miundo mbali mbali kama ifatavyo: Ring (estring) Hii inakua ni kitu cha duara kama ...