FAHAMU KUHUSU PEP DAWA ZITUMIKAZO KUZUIA MAAMBUKIZI YA VVU
Je, utafanya nini Iwapo kinga ilipasuka wakati wa kujamiiana au unafikiri umeambukizwa VVU kwa namna nyingine?.
PEP (Post Exposure Prophylaxis), hutumika ndani ya masaa 72 baada ya kujamiana na mtu mwenye VVU.
Unaweza kupata PEP kutoka kliniki iliyopo karibu nawe.
KUFANYA KAZI,
PEP lazima ianzishwe kabla ya masaa 72 (siku 3) zimepita baada ya kufanya ngono na mwenye VVU.
Vidonge vya PEP vinapaswa kunywewa kila siku kwa mwezi mmoja.
MAUDHI MADOGO MADOGO
Vidonge hivi vya PEP vinaweza kusababisha madhara fulani kama kichefuchefu au kizunguzungu ambacho kinaweza kufanya vigumu kunywa dawa.
Baada ya mwezi mmoja utapima tena VVU ili uhakikishe kuwa bado haujaathirika na VVU.
Comments
Post a Comment